Sera ya Faragha ya WA Notify

Sera hii ya faragha inatumika kwa WA Notify (Arifu WA), teknolojia rasmi ya taarifa ya mfiduo ya Jimbo la Washington. WA Notify iliundwa kwa usimamizi na pendekezo la Department of Health (DOH, Idara ya Afya) ya Jimbo la Washington.

Tunakusanya na kutumia taarifa gani?

Data inayofuata inaweza kukusanywa katika WA Notify:

  • Kupakua au kuwezesha WA Notify.
  • Kupokea taarifa ya mfiduo.
  • Kuwasilisha msimbo wa uthibitishaji au kiungo cha uthibitishaji.
  • Kupakia misimbo nasibu ya watumiaji walioambukizwa ambao wamechagua kuwaarifu wengine.

Department of Health (DOH, Idara ya Afya) katika Jimbo la Washington hutumia taarifa ya tukio a hapo juu kufahamu jinsi ambavyo WA Notify inatumika. Data hii inaweza kushirikiwa na DOH, taasisi za afya ya umma, au mamlaka ya afya yaliyoruhusiwa. Inaweza pia kutumika kwa njia ya pamoja katika malengo ya utafiti wa kitakwimu au kisayansi. Taarifa hii haijumuishi taarifa yoyote ya kibinafsi au ya eneo wala haitatumika kutambua mtumiaji yeyote wa WA Notify.

Ili kulandanisha na lengo la Google na Apple, WA Notify imeundwa ili kulinda faragha ya mtumiaji kama kipaumbele cha juu. WA Notify huzalisha vipengele hivi vya data, ambavyo havina data inayoweza kutambua:

Misimbo Nasibu.

  • Misimbo nasibu inashirikiwa kupitia Bluetooth kati ya simu mahiri za watumiaji wa WA Notify wakiwa karibu na kila mmoja.
  • Misimbo nasibu inazalishwa na kuhifadhiwa kwenye simu janja, si na WA Notify
  • Misimbo nasibu inatumika tu kuruhusu WA Notify na simu yako janja kuangalia iwapo kuna mifiduo ya COVID-19 inayowezekana.
  • Misimbo nasibu inahifadhiwa kwa kipindi kisichozidi siku 14.

Misimbo na viungo vya uthibitishaji

  • Iwapo umeambukizwa ugonjwa COVID-19, na mtu kutoka mamlaka yako ya ndani ya afya ya umma amewasiliana nawe, watauliza iwapo unatumia WA Notify. Iwapo unatumia, watakupatia msimbo au kiungo cha uthibitishaji ili uingize katika WA Notify.
  • DOH pia hutuma taarifa ibukizi na/au ujumbe wa matini ulio na kiungo cha uthibitishaji kwa kila mtu ambao hivi karibuni walipatikana na maambukizo ya COVID-19 ili watumiaji wa WA Notify waweze kuwaarifu watumiaji wengine kwa haraka na bila kujulikana kuhusu mfiduo.
    • Kudonoa taarifa au kubofya kwenye kiungo chako cha uthibitishaji huruhusu misimbo yako nasibu ya kushirikiwa ili watumiaji wengine wa WA Notify ambao ulikuwa karibu nao wanaarifiwa bila kutaja majina kuwa huenda wameambukizwa.
    • DOH hutuma ujumbe wa matini ulio na kiungo cha uthibitishaji kwa kila mtu anayepatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa sababu hatujui anayetumia WA Notify. Ikiwa hutumii WA Notify, unaweza kupuuza ujumbe huo.
    • Unaamua kama utadonoa taarifa au kubofya kwenye kiungo cha uthibitishaji ili kuarifu bila kujilikana watumiaji wengine wa WA Notify.

Kumbukumbu za Matumizi

  • Sawa na karibu kila programu au huduma yoyote ya intaneti, WA Notify huzalisha otomatiki kumbukumbu ukitumia huduma. Kumbukumbu hizi zinajumuisha maelezo kuhusu simu yako janja. Tunatumia maelezo haya kutatua masuala na WA Notify.
  • Kumbukumbu hizi hazijumuishi misimbo nasibu au viungo au misimbo ya uthibitishaji na haziwezi kutumika kufunga ama aina ya msimbo na wewe au simu yako mahiri.
  • Kumbukumbu hizi zinafutwa otomatiki siku 14 baada ya kuzalishwa.

Data ya Uchanganuzi

  • Ukichagua kuwezesha uchanganuzi wa ziada, jumla ya data yenye kikomo itashirikiwa na DOH ili kusaidia kuboresha programu hiyo.
  • Data hii inajumuisha takwimu kuhusu jinsi programu hiyo inatumika. Haijumuishi maelezo yoyote yanayoweza kutumika kukutambua.
  • Unaweza kuchagua kutoshiriki data hii kwa kuzima kushiriki uchanganuzi katika programu hiyo.

Kwa muundo, WA Notify haikusanyi data ya eneo kutoka kwa simu yako janja, na haikusanyi au kushiriki maelezo ambayo yanakufunganisha au kufunganisha simu yako janja kwa misimbo nasibu au misimbo ya uthibitishaji.

Ni nini hufanyika ukiomba msimbo wa uthibitishaji:

Watumiaji wa WA Notify ambao kipimo cha kujipima nyumbani kinaonyesha kuwa wameambukizwa COVID-19 wanaweza kuomba msimbo wa uthibitishaji katika WA Notify ili kuwaarifu bila kujulikana watumiaji wengine wa WA Notify. Ili kupokea msimbo wa uthibitishaji, watumiaji wa WA Notify ni lazima waweke tarehe ya kipimo chao kinachoonyesha wameambukizwa na nambari yao ya simu. Kifaa kilichotumika kuomba msimbo ni lazima kitumike kuweka msimbo wa uthibitishaji au kubofya kiungo cha uthibitishaji ili kuarifu bila kujilikana watumiaji wengine wa WA Notify.

Ili kuzuia ripoti marudufu za matokeo sawa ya kipimo, WA Notify huhifadhi kwa muda mfupi toleo lililolindwa la nambari ya simu iliyotumika kuomba msimbo kwa hadi siku 90. Taarifa hii haitajumuisha taarifa yoyote ya kibinafsi au ya eneo wala haitatumika kutambua mtumiaji yeyote wa WA Notify.

Tunashiriki maelezo yako wakati gani?

Hatutakusanya au kushiriki kwa hiari yoyote kati ya maelezo yako na mtu yeyote, isipokuwa ukichagua kuingiza msimbo wa uthibitishaji au kubofya kiungo cha uthibitishaji. Ukifanya hivyo, WA Notify itashiriki misimbo yako nasibu na simu janja nyingine ambazo zimekuwa karibu na simu yako janja. Kiungo au msimbo wa uthibitishaji hauwezi kuunganishwa tena na wewe na mtu ambaye hana ufikiaji wa simu yako janja. Tafadhali kagua sehemu ya "Tunakusanya na Kutumia Taarifa Gani?" ili kujifunza zaidi kuhusu taarifa ambayo inakusanywa na kutumika katika WA Notify.

Tunalinda vipi maelezo yako?

WA Notify inalinda misimbo nasibu kwa kutumia Exposure Notification Framework (Mfumo wa Taarifa ya Mfiduo) wa Google na Apple, ambao unajumuisha mahitaji maalum zaidi kuhusu jinsi ya kusimbua fiche na kuzihamisha. WA Notify haihifadhi au kuzalisha misimbo yako nasibu - simu yako janja hufanya hivyo.

Haki zako ni taarifa yako

Kwa sababu misimbo ya uthibitishaji na kumbukumbu za programu haziwezi kuhusishwa na wewe bila kufikia simu yako mahiri, DOH haina jia yoyote ya kufikia taarifa hii. Kwa sababu ya hii, DOH haiwezi kukupatia taarifa hii salama au kuifuta iwapo utaomba. Unadhibiti matumizi ya WA Notify. Simu yako janja inafaa kukuruhusu kuzima taarifa za mfiduo au kufuta kumbukumbu za mfiduo kwenye simu yako janja wakati wowote. Zaidi ya hayo, unaweza kuondoa WA Notify wakati wowote ule. Ukiondoa, misimbo yote nasibu iliyohifadhiwa itafutwa.